Tuesday 20 December 2011

Tutumie nafasi hii adimu kukuza utalii wetu watanzania.

Hima hima watanzania na wadau wenzangu,tuliungoja kwa muda mrefu wakati muafaka kama huu!!Kama jirani zetu mlima wa kilimanjaro wanadai uko kwao na mbuga ya serengeti pia,kwanini na sisi wakati huu
ambapo hata hao wageni wanaoambiwa vivutio hivyo nilivyo vitaja vipo katika nchi hiyo ya jirani,sasa wamesusia kwenda huko kwa kuhofia usalama wao hasa baada ya jirani zetu hao kuingia katika mapigano
na jirani zao wasomali.Tuchangamkie hiyo tenda kwa kuboresha huduma zetu kwa wageni,na kuongeza
ukarimu halikadhalika tukiimarisha ulinzi kwa wageni na mali zao,pamoja na kuulinda na kuimarisha amani
yetu kwani hiyo ndio tunu inayotamaniwa na wengi hasa majirani zetu ambao kwao kila kukicha ni vurugu
tupu! Vivutio tulivyo nanvyo nchini kwetu ni mtaji tosha,iweje hao wasio na mitaji watushinde kwa kungangania vyetu? Tuwaonyeshe sasa kwamba tumeamka na tunaweza. Mnasemaje wadau wenzangu?!!

No comments:

Post a Comment